Habari RFI-Ki ni kipindi cha kila siku cha RFI Kiswahili kinachowapa wasikilizaji nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu habari zilizopewa uzito mkubwa katika siku husika. Kila siku mada kuu ya habari inachaguliwa na wasikilizaji wanahimizwa kujadili na kutoa mtazamo wao. Ushiriki hufanyika kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) na pia kwa kupiga simu moja kwa moja. Kipindi hiki ni sehemu ya huduma ya Kiswahili ya Radio France Internationale (RFI).
Épisodes

Kenya: Bunge kujadili mswaada wa kudhibiti mitandao
Nchini Kenya, mswaada umewasilishwa bungeni unaolenga kushinikiza mitandao ya kijamii kudhibiti maudhui hasi kuwafikia watoto chini ya umri wa miaka 18, au kutozwa dolla millioni 3 iwapo itakiuka sheria hiyo, hatua kama hii imechukuliwa na bara ulaya Je unahisi hatua hii itafaulu kudhibiti athari za mitandao ya kijamii kwa watoto ? Skiza makala.

Kenya : Paul Mackenzie afungwa jela miaka 200
Wiki iliyopita Mahakama nchini Kenya, ilimuhukumu kifungo cha miaka 200 mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie, baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na mauaji ya shakahola, hukumu iliyoibua hisia mseto. Tuambie unazungumziaje adhabu iliyotolewa na mahakama, unafikiri inatosha? Haya hapa maoni yako.

Kenya: Yaadimisha miaka 63 ya uhuru wake
Taifa la Kenya linaadhimisha miaka 63 ya kuwakumbuka mashujaa waliopigania uhuru wa taifa hilo Tunakuuliza ni njia ipi sahihi ya kuwakumbuka wote waliopigania uhuru barani Afrika ? Skiza makala.

Africa : Umaskini unatatiza bara Africa
Oktoba 17 dunia huadimisha siku ya kumaliza umaskini kwa wote. Bara Africa bado umaskini ni donda sugu, hapa mskilizaji anatoa maoni yake kuhusu swala hilo.

Vijana wengi Afrika hawawezi kumudu majukumu ya kifedha au kuishi maisha mazuri

Aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila aunda chama kipya na waasi wa M23

Raia wengi wa Afrika wanajipata wamesajiliwa kupigana na Urusi kwenye vita Ukraine

Ongezeko la ajali za barabani katika mataifa ya Afrika Mashariki

Mzozo wa Sudan waendelea, kiongozi wa kijeshi akikataa mazungumza na RSF
Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ameapa kuchukua kila sehemu ya ardhi ya nchi yake iliyo chini ya udhibiti wa wapiganaji wa RSF, huku akikataa majadiliano yanayolenga kumaliza vita nchini humo.

Kenya imeripoti maambukizi ya kwanza ya virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo

Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Walimu, kutambua mchango wao katika kujenga jamii
Licha ya hatua zilizopigwa, walimu kwenye nchi nyingi za Afrika wanalipwa mishahara midogo na wanafanya kazi kwenye mazingira magumu.Tunakuuliza je, walimu wanathaminiwa vya kutosha katika jamii yetu? Nchini mwako hali ikoje na nini kifanyike kuthamini na kuboresha maslahi ya walimu?

Maoni ya wasikilizaji kuhusu matukio mbalimbali ulimwenguni juma hili
Kila siku ya Ijumaa tunakupa nafasi uzungumzie jambo ambalo umeliwazia wiki hii au pia habari kuu ulizozisikia katika matangazo yetu ya juma hili.

Manufaa ya kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu nchini Kenya.
Makala haya yameangazia mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu nchini Kenya, kitakachojengwa na Bilionea wa Afrika, Aliko Dangote, kiwanda hiki kikitarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu na kitagharimu Dola za Marekani Bilioni 16. Tumeuliza msikilizaji anazungumziaje uwekezaji huu, hasa kwakuwa unafanywa na raia wa Afrika.

Mbona matukio ya ukatili na mauaji ya wanawake yameongezeka Afrika?
Wiki hii visa vya wanawake kudhulumiwa na kuuwawa katika baadhi ya mataifa ya Afrika vimekuwa vikiongezeka, matukio ya karibuni ni kupatikana kwa miili zaidi ya 11 ya wanawake waliouawa nchini Afrika Kusini. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanazitaka nchi kukomesha vitendo hivyo. Tumemuuliza msikilizaji wa RFI Kiswahili, anafikiri kwa nini licha ya karne tuliyoko matukio ya ukatili wa wanawa

Hatua ya rais Salva Kiir kuvunja serikali ya mpito kuelekea uchaguzi wa Disemba

Wafanyakazi wa umma hadi elfu 10 nchini Kenya walipata ajira kwa udanganyifu
Idadi kubwa ni wale ambao wameajiriwa na bunge na tume ya uchaguzi na mipaka

Viongozi wa dunia wanakutana wiki hii kwa kikao cha kila mwaka cha UNGA
Idadi kubwa ni wale ambao wameajiriwa na bunge na tume ya uchaguzi na mipaka ,IEBC.

Siku ya kimataifa ya Amani inamaana kwa wananchi wengi ?

Maoni yako kuhusu maangazo yetu juma hili
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakuja nafasi kuchangia mada yoyote kwenye kipindi cha Habari Rafiki.

Kenya kuandaa mashindano ya riadha ya dunia
Kenya imeteuliwa kuandaa mashinda ya dunia ya riadha. Skiza maoni ya mskilizaji.

DRC : Upinzani wapinga mpango wa serikali kubadili katiba
Upinzani nchini DRC wapinga mpango wa serikali kurekebisha katiba Shabarikiliza maoni ya mskilizaji .

Kenya : Raia wa Burundi wazidi kuondoka nchini Kenya
Raia wa Burundi wanaofanya baishara ndogondogo nchini Kenya, wamendelea kuondoka nchini humo kutokana tangazo la rais William Ruto kuwataka wageni kusajili biashara zao. Skiza maoni ya mskilizaji.

EAC : Mvua za El Nino zatarajaiwa
Darubini yetu inalenga kanda ya Africa Masharaiki ambapo watalaam wa utabiri wa hali ya hewa wanaonya kuwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, zitashuhudia EL Nino kati ya mwezi Oktoba hadi Desemba, ambako mvua kubwa inatarajiwa kunyesha. Umejiandaa vipi kukabiliana na EL Nino ? Skiza maoni ya mskilizaji.

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuhamasisha kuzuia visa vya watu kujiuwa.
Shirika la afya duniani WHO linasema watu laki 7 na elfu 20 hujitoa uhai kila mwaka. Kujiua ni kati ya sababu tatu kuu ya vifo miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15–29.











