Accueil Podcasts Siha Njema
Siha Njema

Siha Njema

RFI Kiswahili 24 Épisodes sept. 19, 2026

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Épisodes

Kwa nini kilimo sharti kuzingatiwa kumaliza njaa barani Afrika
Kwa nini kilimo sharti kuzingatiwa kumaliza njaa barani Afrika sept. 19, 2026 00:09:48 Ripoti ya mashirika kadhaa ya umoja wa mataifa yameonesha Afrika bado ina watu wengi ambao wanakabiliwa na njaa. Hii ni licha ya Afrika kuwa sehemu inayofanya kilimo . Watalaam wanasema kilimo kimeathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi  kama vile mafuriko,ukame na sasa hivi vijana wengi hawapendi kilimo Hivi basi nini kifanyike kuhakikisha kuwa kuna lishe bora barani Afrika? Dkt Calistus K
Kisukari inaendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wa macho nchini Kenya
Kisukari inaendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wa macho nchini Kenya sept. 9, 2026 00:10:10 Magonjwa yanoyohitaji matibabu ya muda mrefu ukiwemo kisukari unaendelea kusababisha watu wengi kupata matatizo ya macho au kupoteza uwezo wa kuona
Afrika kukabiliana na usugu wa vimelea vifo vikitarajiwa kuvuka milioni 4
Afrika kukabiliana na usugu wa vimelea vifo vikitarajiwa kuvuka milioni 4 sept. 2, 2026 00:10:07 Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika ,Africa CDC kimeonya vifo vinavyohusishwa na usugu wa vimelea vinatarajiwa kuvuka milioni 4 mwaka wa 2050 Mashirika ya kikanda yanasisitiza utekelezwaji wa pamoja wa mikakati ya kukabiliana na usugu wa vimelea ikiwemo afya ya mifugo ,matumizi mazuri ya dawa za antibiotics na dawa za kunyunyuzia mimea kwenye sekta ya kilimo.   Watalaam wa afya wa
Mapambano dhidi ya Ebola Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Mapambano dhidi ya Ebola Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo août 28, 2026 00:09:41 Ebola imekamilisha siku 100 tangu ilipotangazwa na bado bado haijadhibitiwa Shirika la kimataifa la VillageReach miongoni mwa mashirika yaliyoalikwa na utawala wa Kinshasa kusaidia juhudi za kudhibiti mwambao hatari wa Ebola Bundibugyo linazungumzia kuhusu mapambano hayo. Baadhi ya changamoto zinazofanya ugumu mapambano hayo ni ukosefu wa uaminifu kati ya wananchi na serikali ,tamaduni na pia taar
Kwa nini bima ya afya ya msafiri ni sharti muhimu kwa mataifa ya Afrika
Kwa nini bima ya afya ya msafiri ni sharti muhimu kwa mataifa ya Afrika août 18, 2026 00:10:01 Umuhimu wa bima ya afya kwa wasafiri ni pamoja na kupunguza gharama kwa taifa mwenyeji haswa wakati huu nchi nyingi hususan za Afrika zinashuhudia ongezeko la milipuko wa magonjwa ya milipuko Sharti hilo pia linatoa fursa kwa nchi kuboresha mifumo ya afya ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaohitaji huduma za afya kwa nchi wanazozitembelea.
Unaweza  kuendelea kunyonyesha hata baada ya kutenganishwa kwa muda na mwanao
Unaweza kuendelea kunyonyesha hata baada ya kutenganishwa kwa muda na mwanao août 11, 2026 00:09:44 Imani kuwa mama na mtoto wanapotenganishwa inaweza kuathiri ubora wa maziwa ya mama inapotosha. Watalaam wanasisitiza maziwa ya mama hayawezi kuharibika kwenye titi. Aidha kunyonyesha kwa uaminifu kunaweza kukuepusha na saratani na mbinu pia ya kupanga uzazi.
Kwa nini   watalaam wanahoji maumivu  makali wakati wa hedhi si kawaida
Kwa nini watalaam wanahoji maumivu makali wakati wa hedhi si kawaida juil. 31, 2026 00:09:52 Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.
Changamoto ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa
Changamoto ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa juil. 21, 2026 00:10:09 Raia mmoja wa Kenya amefika kwenye bunge la kitaifa nchini Kenya akitaka swala la wanaume na wanawake kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kuorodheshwa kuwa ulemavu Kwa mujibu wa daktari Dominic Osiemo ,tatizo hilo linachangiwa na maswala kadhaa yakiwemo matumizi ya dawa za kisukari ,shinikizo la damu na msongo wa mawazo.
Visa vya kung'atwa na Nyoka vyaongezeka kaunti ya Turkana Nchini Kenya
Visa vya kung'atwa na Nyoka vyaongezeka kaunti ya Turkana Nchini Kenya juil. 21, 2026 00:09:29 Kaunti ya Turkana inaongoza nchini Kenya kwa visa vya watu kung'atwa na nyoka. Wataalamu wa afya wanasema mabadiliko ya tabianchi, joto kali na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya vinaongeza hatari kwa wakazi wa maeneo mengi ya kaunti hiyo,huku shirika la afya duniani WHO likisema visa vya kuumwa na nyoka vinapuuzwa wakati huu karibia watu 32000 wakifariki kila mwaka  kutokana na sumu ya n
Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma
Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma juil. 10, 2026 00:10:09 Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa  na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia  maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea
Kampeni kuhakikisha vyakula  vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya
Kampeni kuhakikisha vyakula vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya juin 30, 2026 00:10:00 Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa  na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi  ya kila mara. Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha  mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya  madini ambavyo  vyakula au vinywaji  vinavyouzwa vinafaa kukidhii  au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,
Kwa nini ni muhimu wanaume kuzingatia afya zao haswa afya ya akili
Kwa nini ni muhimu wanaume kuzingatia afya zao haswa afya ya akili juin 23, 2026 00:09:56 Mwezi Juni ni mwezi wa kutoa uhamasisho kuhusu afya ya akili miongoni mwa wanaume ,swala la afya ambalo hupuuzwa mno Daktari Dominic Osiemo anasema wanaume wana haki wa kuonesha hisia ,kueleza maumivu  yao na kutaka kuskizwa. Na wanapofanya hivyo wanalinda afya zao za akili. Anaonya wanaume wengi wanakuwa hatarini kwa sababu wanajaribu kudhihirishia jamii kuwa wao ni imara siku zote. Baadhi ya vip

Recommandé