
Afrika Ya Mashariki
Kipindi hiki cha Afrika ya Mashariki kinatoa taarifa na elimu kuhusu changamoto za maisha za wananchi wa Afrika Mashariki na eneo la maziwa makuu. Wapendwa wa kipindi wanapata nafasi ya kutoa mawazo yao na kusikiliza wataalamu mbalimbali. Lengo ni kuwasaidia kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Épisodes

EAC: Kesi za kisiasa au utawala wa kisheria
Katika kipindi cha miaka ya karibuni, viongozi wa upinzani katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki wameendelea kujikuta mahakamani wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo uhaini. katika Makala ya Afrika Mashariki, tunaangazia mwenendo wa kesi zinazowakabili viongozi wa upinzani katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, je, ni ishara ya kuimarika kwa utawala wa sheria au kuna maswali yanay

Kenya yaanza safari ya kutafuta dira mpya, ruwaza ya 2030 ikielekea kufika ukomo
Kenya imeanza safari ya kutafuta dira mpya ya maendeleo baada ya Ruwaza ya Taifa ya Maendeleo 2030 kuelekea kufikia ukomo wake. Safari hii inakuja wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, ikiwa na dira yake ya pamoja ya mwaka 2050, inayolenga kujenga ukanda wenye uchumi shindani, miundombinu iliyounganishwa, viwanda, biashara, ajira na maendeleo ya watu.

Tanzania: Nanenane imebaki maonesho ya kilimo au imegeuka soko la biashara?
Tunaangazia mjadala kuhusu mustakabali wa maonesho ya nanenane nchini Tanzania. Je yaendelee kuwa jukwaa la teknolojia za kilimo pekee au yafungue milango kwa biashara zote?

Safari ya Tohara ya kitabibu kutoka mila hadi afya ya umma
Katika Makala ya wiki hii, tunaangazia safari ya Tohara ya kitabibu kutoka mila hadi afya ya umma.

Mazungumzo ya kitaifa yanaweza kuponya majeraha ya DRC?
Katika Makala ya Afrika Mashariki, tunaangazia mchakato wa mazungumzo ya kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nafasi ya viongozi wa dini na matarajio ya wadau wa kisiasa katika kutafuta amani na maridhiano ya kudumu.

CCM na ACT-Wazalendo vimesaini makubaliano mapya ya maridhiano.
Baada ya mvutano wa kisiasa uliojitokeza mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita huko Zanzibar, sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo vimesaini makubaliano mapya ya maridhiano. Lakini je, makubaliano hayo yatafungua ukurasa mpya wa demokrasia, au ni hatua ya kujenga utulivu kuelekea uchaguzi ujao? Makubaliano hayo yaliyosainiwa Julai 9, 2026 yanajumuisha mapitio ya Katiba, mageuzi ya uchagu

Hali ya Ziwa Victoria na changamoto zinazolikabili
Tunaangazia hali ya Ziwa Victoria, changamoto zinazolikabili pamoja na juhudi za kikanda zinazofanyika kulinusuru ziwa hilo ambalo ni mhimili wa uchumi na maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki. Ziwa Victoria, ambalo ni tegemeo la mamilioni ya wananchi wa Afrika Mashariki, linaendelea kukumbwa na changamoto kubwa za mazingira, uvuvi haramu na uchafuzi wa maji. Ripoti mpya ya mwaka 2025 imeonya kuw

Tanzania: Ripoti ya Tume ya uchunguzi kuhusu vurugu za uchaguzi mkuu wa Oktoba
Makala ya Afrika Mashariki, ikiangazia juu ya ripoti ya Tume ya uchunguzi wa matukio ya wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa October 29, 2025 nchini Tanzania.

Kumbukizi ya miaka 32 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994
April 7, 1994 ni siku ya ambayo historia ya Rwanda ilianadikwa kwa wino mwekundu kumaanisha hatari, kifo cha Rais zamani wa Taifa hilo Juvenal Habyarimana aliuawa akitokea nchini Tanzania katika mchakato wa kusaka amani nchini Rwanda, baada ya waasi wa kundi la RPF wakati huo, ambalo kwa sasa ni chama kilichopo madarakani, kuanzisha vita dhidi ya serikali ya Juvenal Habyarimana, wakimtuhumu kuwate

Kasi na mapokeo ya ueneaji wa akili mnemba barani Afrika
Karibu katika ya Afrika mashariki hii leo macho na masikio ya Makala haya yanatazama kasi na mapokeo ya ueneaji wa akili mnemba barani Afrika tukienega katika Mkutano wa Kimataifa wa AI kuhusu Afrika 2025, unaofanyika Kigali nchini Rwanda Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe soote hadi tamati

Je una ufahamu juu ya ulinzi wa taarifa binafsi ?
Kasi ya ugunduzi na uvumbuzi katika maswala ya sayansi na teknolojia na ujio wa Internet sanjali na matumzi ya mitandao ya kijamii yanafanya wajamii kuwa katika hatari kumbwa kupoteza usiri wa taarifa zao. Baada ya mabadiliko makubwa ya teknolojia yamesababisha taarifa za watu kuwa ni moja ya mtaji mkubwa kwa watu wengine na makampuni makubwa Tanzania kama yalivyo mataifa mengine ya Afrika mashar

Tatizo la kifua kikuu (TB) katika mataifa ya Afrika Mashariki
Maambukizi ya kifua kikuu yanaweza kuenezwa kwa urahisi katika miji mikubwa na maeneo ya umma ambapo kuna mkusanyiko mkubwa wa watu, kama vile vituo vya mabasi, masoko, na hata sehemu za kazi kama waendesha bodaboda wanavyojihusisha. Msikilizaji wa RFI Kiswahili karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwana kuangaza namna waendesha bodaboda wanaweza kuchukua tahadhari ya kupambana

Tanzania: Namna wakaazi wa vijijini wanafikiwa na huduma za maji
Namna wakazi wa maeneo ya vijijini wanafikiwa na huduma za maji nchini Tanzania.

Athari za mgogoro wa DRC katika mataifa ya Afrika
Mgogoro wa Mashariki ya DRC umeendelea kwa miongo kadhaa, na bado ni moja ya changamoto kubwa za kiusalama na kisiasa Barani Afrika. Katika Mashariki ya DRC, kuna makundi ya waasi kama vile M23, ADF, Twirwaneho, ambayo yameongeza umwagaji damu na kusababisha maelfu ya watu kuhama kutoka maeneo yao.Siasa za kikanda, ushindani wa madaraka kati ya mataifa kama Rwanda yana iweka DRC njia panda kila uc

Umuhimu wa kutunza lugha mama katika jamii za Afrika
Karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tukiangaza safari ya miaka 25 ya UNESCO kuenzi lugha mama na nafasi ya lugha mama katika kukuza maendeleo ya jamii Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati ya Makala haya. Lugha ni muhimu kwa elimu na maendeleo endelevu, zikitumika kama njia kuu ambayo maarifa hupitishwa na tamaduni kuhifadhiwa. Kwa muj

Namna wakazi wanaoishi karibu na migodi wanaweza kufaidika na shughuli hizo
Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama na kuangazia kwa namna gani wakazi wanaozunguka migodi ya madini kupitia uwajibikaji kwa jamii. Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekua, na kukua huku ni kutokana na ongezeko la asilimia 7.3 kwa mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9. Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii serikali ya Tanzania imechukua hatua muhimu ya kuhakikisha kwamba waweke

Tanzania: Changamoto wanazokabiliwa nazo watu wenye Albinism mjini Mwanza
Watu wenye ualbino Afrika Mashariki, na hasa nchini Tanzania, wanakutana na changamoto kubwa za kijamii, kisiasa na kiuchumi. Vilevile, wanakumbana na unyanyapaa, ubaguzi, na vitendo vya kikatili vinavyoweza kupelekea madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na mauaji na uharibifu wa miili yao. Ingawa jamii ya watu wenye ualbino imekuwa na umakini wa kimataifa, bado wanakumbana na hatari na shida kubwa,

Safari ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Zanzibar ilipata uhuru kamili mnamo Desemba 10, 1963, kutoka kwa Uingereza, Waarabu walio wachache walifanikiwa kushika madaraka waliyorithi kutoka kwa Zanzibar kuwepo kama eneo la ng'ambo la Oman.

Tanzania: Kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa
Wiki hii tunatuwa nchini Tanzania tukiangaza kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa (UVIDA)

Uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani Arusha Kaskazini mwa Tanzania
Sekta ya Kilimo inaongoza kuwa na fursa nyingi za uwekezaji kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwa mfano uzalishaji wa Ngano, mafuta ya kupikia, matunda na mboga mboga, mbolea, Viatilifu, mbegu bora, vifungashio, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno na eneo la kilimo cha umwagiliaji.

Tanzania: Kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya majimaji
Karibu katika Makala ya Afrika mashariki, hii leo tunatuwama nchini Tanzania katika Mkoa Lindi uliopo kusini mwa Tanzania mahali ilipo ibuka vita vya majimaji mara hii ikiwa ni kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya Majimaji. Vita vya Majimaji vilipata mizizi yake katika eneo la Nandete Kipatimu, ambapo jamii za Matumbi zilijitokeza kwa ujasiri dhidi ya ukandamizaji wa kikoloni.Roho hii

Wiki ya vijana ilivyoaadhimishwa mjini Mwanza nchini Tanzania
Tunaangazia jinsi vijana wanavyoweza kutumia fursa za kidijitali katika kukuza na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi mjini Mwanza nchini Tanzania.

Tanzania: Mradi wa Jenga Kesho Bora ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samaki
Namna Mradi wa Jenga Kesho Bora (BBT), unaosimamiwa na Wizara ya Kilimo nchini Tanzania ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria.

Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya lugha ya alama
Jamii imetakiwa kujifunza lugha ya alama ilikuweza kuwasiliana vyema na watu wanaoishi na ulemavu wa kusikia.
Recommandé

Aprende Francés con Claudia En Francia

Interlude Hip-Hop Classics

C'est bon à savoir

L'antre de la peur

Les Nouilles Rampantes

La Station Hantée

ITMPROD en Mix Live set dj-Radio
Devenir iconique

Cahier de Brouillon

Sexualité: mode d'emploi

C'est creepy - serial killers, paranormal, mystères

Les podcasts du Média