
Gurudumu la Uchumi
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza.
Épisodes

Maisha mapya: Jinsi akina mama vijana wanavyobadilisha ujuzi kuwa fursa
Nchini Kenya, suala la mimba za utotoni ni changamoto. Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya taofa nchini Kenya kupitia utafiti wa mwaka 2022 asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 walikuwa wamewahi kupata ujauzito. Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii, tunaangazia namna akina mama hawa wanavyogeuza ujuzi, juhudi na fursa za kiuchumi kuwa njia ya kujitegemea na kuwajengea wato

Umeme unaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki?
Wikendi iliyopita, Tanzania ilizundua rasmi Mradi wa Umeme wa Maji wa bwawa la Julius Nyerere, lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115. Mradi huu, uliogharimu takribani shilingi trilioni 7.45 za Tanzania sawa na karibu dola za Marekani bilioni 2.9, unaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme. Katika Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunajiuluza Je, megawati hizi zitageuka ku

Goma: Wanawake wapambana na umaskini licha ya changamoto za usalama.
Msikilizaji katika mazingira ambayo migogoro na changamoto za kiuchumi zimeathiri maisha ya kila siku ya wananchi, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta njia mbadala za kujipatia kipato na kuendesha familia zao.Hali hii inashuhudiwa katika mji wa Goma, mashariki mwa DRC, ambako baadhi ya wanawake wamegeukia ufugaji wa kuku kama njia ya kujikimu, hasa baada ya shughuli za baadhi ya taasisi za kifedha

Je, Nchi Inaweza Kuendelea Bila Dira ya Maendeleo?
Msikilizaji taifa linaweza kuishi siku moja baada ya nyingine bila kujua linaelekea wapi. Lakini taifa linalotaka kujenga uchumi imara, ajira bora na maisha bora kwa wananchi wake, linahitaji zaidi ya mipango ya leo, kwa kifupî linahitaji dira. Kwenye makala ya wiki hii tunaangazia dira ya taifa ni nini.

Sehemu ya Pili: Hatifungani ni nini na kwanini inakuhusu
Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

Hatifungani za serikali na hazina: Kwa nini zinahusu kila mwananchi?
Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

Migogoro ya kimataifa inavyoathiri uchumi wa wananchi Afrika
Katika Makala haya hivi leo tunajadili uhusiano kati ya siasa za kimataifa na uchumi wa wananchi wa Afrika, mara yingi tunasikia taarifa za vita, migogoro ya kisiasa au mivutano kati ya mataifa makubwa kama Urusi na Ukraine, Mashariki ya Kati, au migogoro inayovuruga usafirishaji wa bidhaa duniani. Kuzungumzia hili, hivi leo nimemualika Safari Fungo, mtaalamu wa masuala ya uchumi, utangamano wa ki

Sarafu za kidijitali ‘Cryptocurrency’ uwekezaji wa kisasa wenye fursa na hatari
Katika miaka ya hivi karibuni, sarafu za kidijitali maarufu kama cryptocurrency zimezidi kuvutia watu wengi duniani. Wapo waliopata faida kubwa, lakini pia wapo waliopoteza fedha nyingi kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu hizo. Leo katika Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza: Je, sarafu za kidijitali ‘cryptocurrency’ ni uwekezaji wa kweli, au ni uwekezaji wenye hatari kubwa ambao watu w

Kodi na Maendeleo: Je, tunapata thamani ya kodi tunazolipa?
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo, tunajadili nafasi ya kodi katika maendeleo ya uchumi, umuhimu wa kulipa kodi, na jinsi serikali na wananchi wanavyoweza kushirikiana kujenga uchumi imara na wenye manufaa kwa wote.

Je, kukopa kunasaidia ukuaji wa uchumi au kunaleta hatari za siku zijazo?
Msikilizaji nchi nyingi za Afrika Mashariki zimeendelea kukopa ili kufadhili maendeleo, na huku wadau wengine wakisema mikopo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, Wengine wanaonya kuwa madeni yanapoongezeka kupita kiasi, serikali hulazimika kutumia fedha nyingi kulipa madeni hayo badala ya kuboresha huduma muhimu kama vile afya, elimu na ajira. Katika Makala ya Gurumu la Uchumi hivi leo, tunauliza: Je,

Kutoka taslimu hadi kidijitali: Namna simu zinavyobadili mfumo wa malipo Afrika
Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia. Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya telknoloj

Sekta ya maua Kenya yatikiswa na gharama na kuyumba kwa masoko ya kimataifa
Msikilizaji Sekta ya maua nchini Kenya, ambayo kwa muda mrefu imekuwa miongoni mwa nguzo muhimu za uchumi na chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni, ikiingizia nchi zaidi ya dola bilioni moja za Marekani kila mwaka, sasa inakabiliwa na changamoto zinazotia wasiwasi kuhusu mustakabali wake.

Umuhimu wa bara la Afrika kufanya biashara za ndani
Katika makala ya wiki hii, tunajadili ni kwanini nchi za Afrika zinapaswa kuongeza kasi ya ufanyaji wa biashara za wenyewe kwa wenyewe kukuza utangamano wa kikanda.

Mkutano wa 'Africa Forward' una maana gani kwa mustakabali wa Afrika
Tarehe 11 na 12 ya wiki ijayo, Jiji la Nairobi, Kenya litakuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kihistoria wa ‘Africa Forward’ kati ya Ufaransa na Afrika, mkutano ambao unafanyika kwenye nchi inazungumza Kingereza, ambapo viongozi wa Afrika, wafanyabiashara na wabunifu vijana kutoka Afrika na Ufaransa watakongamana kwa siku mbili. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo tunaangazia uhusiano m

Akili unde na mustakabali wa uchumi wa Afrika: Fursa mpya kwa vijana wabunifu
Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa.Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambaye

Kwa nini vikwazo vya usafirishaji ni kizuizi kikubwa cha biashara Afrika Mashariki
Kupitia ripoti iliyozinduliwa juma hili na shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, inaonyesha kuwa kusafirisha bidhaa katika njia muhimu za biashara za Afrika bado ni ghali na haitabiriki, ambapo wakati mwingine hugharimu hadi dola 7,000 za Marekani kwa kontena moja kati ya Nairobi na Lusaka. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tumezungumza na Tobias Alando, mkurugenzi mtendaji wa shiri

Uwazi kwenye ubinafsishaji wa mashirika ya uma ni muhimu kwa maendeleo
Msikilizaji Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikifanya mageuzi makubwa ya kiuchumi. Mojawapo ya mageuzi hayo ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Leo tunajiuliza, Je, ubinafsishaji ni kweli unasaidia uchumi kukua, au serikali inapaswa kubaki na umiliki wa mashirika muhimu?

Vita ya Iran: Afrika imejipangaje kukabiliana na athari za kiuchumi
Msikilizaji mara zote mgogoro wa mashariki ya kati, umekuwa na athari hasi za kiuchumi na biashara duniani, Swali kubwa tunajiuliza hivi leo ni Je, Afrika iko salama kiasi gani? Vita hivi vitaathiri vipi uchumi wa dunia — na gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida barani Afrika?

Ushirikishwaji wa wanawake katika sekta za kiuchumi chanzo cha ukuaji wa uchumi
Benki ya Dunia inasema hata katika nchi zenye sheria za kisasa kuhusu usawa kazini, nchi hizo zimeshindwa kuzitekeleza, hadi sasa hakuna nchi iliyofikia kiwango cha juu cha usawa kazini, n ani asilimia kidogo tu ya wanawake wanaishi kwenye nchi zenye angalau sheria bora, huku mataifa 70 ikiwemo Misri, Madagascra na Somalia zikipiga hatua katika kuboresha mazingira ya usawa kati yam waka 2023 na 20

Ushirikiano wa kikanda hatarini: Nakisi ya bajeti yaibua maswali mapya
Juma hili tunajadili kuhusu mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa wakati huu kukiwa na taarifa kuwa inakabiliwa na mgogoro wa kifedha. Taarifa zinaonesha kuwa Jumuiya hiyo inakabiliwa na upungufu wa bajeti unaofikia karibu dola za marekani milioni 89, pengo ambalo huenda likatatiza shughuli za Jumuiya hiyo, jambo ambalo limemfanya rais wa Kenya William Ruto ambaye ni mwenyekiti wa jumui

Dubai: Viongozi wa dunia waangazia mageuzi ya sera, ubunifu na mifumo mipya ya utawala
Mkutano wa siku tatu wa Serikali za Dunia mwaka 2026 huko Dubai umesisitiza kuhusu udhibiti wa Akili Mnemba, AI, mageuzi ya kidijitali, uchumi endelevu na thabiti duniani. Viongozi mbalimbali wametoa wito wa kuwepo ushirikiano thabiti wa kimataifa na mifumo mipya ya utawala inayoweza kutazamia changamoto za siku zijazo lakini pia kushughulikia masuala ya pamoja kama vile mabadiliko ya hali ya hew

Ushindani wa mataifa makubwa na mustakabali wa uchumi wa Dunia
Msikilizaji mataifa makubwa kama Marekani, China, Urusi na Ulaya yanaendelea kushindana kiuchumi, kuanzia kwenye biashara, teknolojia, nishati na rasilimali. Lakini je, ushindani wao unaathiri vipi uchumi wa dunia? Leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi tunajadili, “Athari za Kiuchumi kwa Dunia Zitokanazo na Ushindani wa Maslahi ya Kiuchumi kati ya Mataifa Makubwa.”

Kenya Kuwa Singapore ya Afrika: Ndoto au Uhalisia?
Msikilizaji Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kusisitiza azma ya kuifanya nchi yake kuwa Singapore ya Afrika, suala ambalo limeibua mjadala mkali nchini humo baadhi wakisema ni suala ambalo halitawezekana chini ya utawala wake na wengine wakiona ni jambo linalowezekana. Kwenye makala yetu leo tunajiuliza, je, Kenya inaelekea huko? Ndoto hii inawezekana au ni siasa?

Kutoka Ufugaji wa Mifugo hadi Samaki: Mabadiliko ya Kiuchumi Kajiado
Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.
Recommandé

Le débat

Conflits, géopolitique

Esprits Libres

Journal de l'Afrique

C dans l'air

Ingrid Immersion France

Les Aventures d'Ulysse

Le Bureau de l'étrange - ( HISTOIRES D'HORREUR - CREEPYPASTAS - HISTOIRES AUDIOS)

Histoires de lieux hantés

ΦΙΛΟΣΟΦΙΑ - Amour de la sagesse - L'histoire de la philosophie

Ondes sociales

Aprende Francés con Claudia En Francia